For home theatre system solution

Thursday, February 2, 2012

COMING SOON
 MCHEZO MCHAFU
Imeandikwa na: Konzo Kalmas
UTANGULIZI
Dunia ni tambara bovu lenye matundu mengi makubwa na madogo. Ni tambara ambalo halina thamani ya kusadifu ubeleko uwezao kueleka mwana. Aina ya uchafu ambao unalolichafua tambara hili ni kama vile ufuska, rushwa, uasherati, uchawi na ushirikina n.k.
Dunia pia ni uwanja wa fujo . Ni uwanja ambao unawabeba watu wa matabaka mawili tofauti. Matabaka haya ni yale ya watu wenye pesa na wale wasio na pesa. Matendo mengi mabaya na machafu hufanywa katika uwanja huu kwa nguvu  ya pesa. Pesa huzigeuza nyoyo na roho za binadamu na kuzifanya zisiwe na hata chembe ya utu na ubinadamu.
Mchezo wa maisha wa Mr. Mkoma dhidi ya wanadamu wengine uligeuka na kuwa ‘’Mchezo Mchafu’’ Mwamuzi pekee akiwa ni pesa lukuki ziliz hodhiwa na Mr. Mkoma. Roho ya Mr.Mkoma ilikuwa haina tofauti na ile ya mnyama mkali aliyekuwa tayari kumrarua binadamu yeyote na kuitafuna nyama yake pamoja na kuinywa damu yake.
Karibu uungane name katika simulizi hii ya kusisimua na kusikitisha ……..!