For home theatre system solution

Thursday, March 1, 2012

IRINGA

MAKAMU WA RAIS DR. BILAL ASHUHUDIA NGUVU YA CHADEMA JIMBO LA IRINGA MJINI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini, kupitia tiketi ya CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa, wakati akiwa Uwanja wa Ndege wa mkoani Iringa jana akirejea jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza ziara yake ya mkoani humo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
MAKAMU wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilala ashuhudia kifo cha chama cha mapinduzi (CCM) jimbo la Iringa mjini baada ya chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema) wilaya ya Iringa mjini kuwataka wafuasi wa chama hicho walioshiriki mkutano wa hadhara wa makamu huyo wa Rais kuonyesha itikadi yao dhidi ya Chadema.

Makamu wa Rais alishuhudia nguvu hiyo ya chadema baada ya mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Iringa mjini na mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa kutumia jukwaa hilo la Makamu wa Rais kukionya chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa kwa kujimilikisha ziara za viongozi wa serikali kwa kuweka bendera za CCM na kujipigia debe .

" Mheshimiwa makamu wa Rais naomba leo nitoe onyo kwa CCM na kuwaonyesha kuwa si vizuri kuteka misafara ya viongozi wa kitaifa wa serikali wanapokuwa katika ziara mkoani hapa...imekuwa ni kawaida ya CCM kutumia majukwaa haya kujipigia debe sasa naomba uniruhusu kuwasalimu wananchi kwa falsafa ya chama changu cha Chadema .....naomba wananchi wote kunjeni ngumi nikisema peoples semeni Power’ " salamu hiyo ilifanya robo tatu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano huo uliofanyika uwanja wa Mwembetogwa juzi kulipula kwa sauti kubwa na kujibu salamu hiyo 

Hatua ya mbunge Msigwa kumwonyesha makamu wa Rais nguvu ya Chadema ilitokana na na Mkuu wa Wilaya ya Iringa,Kapt. Mstaafu Asseri Msangi kumtaka kupanda jukwaani ili awasalimu wananchi wa Manispaa hiyo kama ilivyokuwa kwa wabunge wa CCM

Baada ya salaam hizo mbunge huyo alimweleza Makamu wa Rais na ujumbe wake kwamba kwa kuwa na yeye (Msigwa) ni Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Iringa, angeamua kuwaambia wananchi wake wabebe bendera zao au kuvalia kombati za chama chake ingekuwa balaa.

“Kama na mimi ningewatuma wananchi wangu wabebe bendera au kuvalia mavazi ya chama (Kombati) ingekuwa balaa lakini naomba niwasalimu wananchi wangu kwa salaamu ya chama chetu…’Iringa, Peoplesssss,wananchi wakaitika Power! huku wakinyoosha vidole viwili juu jambo ambalo lilimlazimu Msigwa kuwaambia wananchi hao, nawaombeni sasa, mumsikilize mheshimiwa Makamu wa Rais,”alisema mbunge huyo.

Hata hivyo CCM kupitia katibu wake wa mkoa Mary Tesha alipanda jukwaani na kutaka kujaribu kuonyesha nguvu ya CCM kwa kusalimia kwa salamu ya CCM na kujibiwa na watu wasio zidi 50 wakiwemo viongozi wa jukwaa kuu huku watu zaidi ya 10000 wakinyamaza kimya na kuzomea .

“CCM Oyeee! Mheshimiwa Makamu wa Rais siyo kweli kwamba tumekuwa tukiteka ziara wala kuipora mikutano ya serikali kwa kuweka bendera zetu.
Hata mheshimiwa mbunge (Msigwa) anajua kwamba Makamu wa Rais amekuja kukagua miradi inayotekelezwa kwa ilani ya CCM,”alisema katibu huyo akijibu kauli iliyotolewa na mbunge wa Iringa mjini (Chadema).

Hata hivyo,katika hali isiyo ya kawaida wakati mbunge huyo akitumia salaam ya Peoples Power, Dk.Bilali alikuwa mtulivu na hakuonekana kuvurugwa na falsafa hiyo hata wakati alipopanda jukwaani kuwahutubia wananchi wa Manispaa ya Iringa waliofika kumsikiliza.

Mbali ya Chadema kuchukizwa na utaratibu huo wa CCM kupeperusha bendera za CCM katika uwanja huo bado Chadema ililazimika kupamba bendera zake kando kando ya barabara ya Kihesa na wakati msafara wa makamu wa Rais uliokuwa na magari zaidi ya 40 ukipita katika eneo hilo kuelekea uwanja wa ndege Nduli ulishuhudia utitiri wa bendera hizo za Chadema .

Chanzo: francisgodwin.blogspot.com