For home theatre system solution

Tuesday, March 6, 2012

NJOMBE


WANAFUNZI WAFANYA MAANDAMANO
Na Kalmas Konzo

Zaidi ya wanafunzi 1000 wa shule za msingi Mpechi na Sabasaba wakiongozana na baadhi ya walimu wa shule hizo pamoja na wazazi wengine walifunga barabara kuu ya Njombe - Songea kwa zaidi ya masaa matatu wakiishinikiza serikali kujenga matuta katika barabara hiyo kwa lengo la kudhibiti ajali za mara kwa mara zinazotokea katika barabara hiyo.

sakata hilo lilianza mara tu baada ya wanafunzi kupata taarifa ya kifo cha mtoto Irene Kadege aliyekuwa akisoma darasa la awali katika shule ya msingi Sabasaba.

Kifo cha mtoto huyo kilitokana na kugongwa na gari lenye namba za usajili T 612 AQP jirani na ofisi za TANESCO Njombe.

Wanafunzi hao waliifunga barabara hiyo huku wakiandamana kutoka maeneo ya shule zao mpaka maeneo ya stendi kuu huku wakiimba nyimbo za kuhamasisha madereva wawe makini wanapoendesha vyombo vya usafiri barabarani.

Hali hiyo ya mtafaruku wa wanafunzi ilikuja kutulizwa na mkuu wa wilaya ya Njombe Mh. saraha Dumba ambaye aliwaahidi wanafunzi hao kwamba suala la kujenga matuta mapema iwezekanavyo ikiwa ni sambaba na kuwaweka askari wa usalama barabarani katika eneo hilo ambao watahakikisha usalama wa waenda kwa miguu.

Kumekuwa na ongezeko la ajali za barabarani katika barabara ya Njombe - Songea hali inayosababishwa na madereva wazembe wanaoshindwa kuzingatia sheria za usalama barabarani.