For home theatre system solution

Thursday, March 22, 2012

MALI

Wanajeshi watangaza mapinduzi Mali

 22 Machi, 2012 - Saa 09:07 GMT

Wanajeshi waasi wametangaza katika televisheni ya taifa ya
Mali kuwa wamechukua udhibiti wa nchi, saa kadha baada ya kuvamia kasri ya rais.
Wanajeshi walioasi wanasema kuna marufuku ya kutotoka nje katika nchi nzima na kwamba katiba haitatumika kwa sasa.
Bamako
Marufuku kutoka nje nchini Mali
Siku ya Jumatano wanajeshi hao walifyatuliana risasi na wanajeshi watiifu kwa serikali.
Wanasema serikali haijawapa silaha za kutosha kukabiliana na waasi wa jamii ya Tuareg.
Tayari walikuwa wamechukua udhibiti wa kituo cha taifa cha redio na televisheni na kusitisha matangazo.

Baada ya saa kadha ya kuonyesha picha za nyimbo za wanamuziki wa Mali, kundi la wanajeshi likaonekana kwenye televisheni mapema siku ya Alhamisi, wakitambulishwa kama "Kamati itakayorudisha Demokrasia na kutuliza hali katika nchi".

Msemaji wa waasi hao, aliyetajwa kwa jina la Luteni Amadou Konare, alisema sasa wamemaliza "utawala usio thabiti" wa Rais Amadou Toumani Toure.

LUDEWA

  •  HATIMAYE DIWANI ALIYEJINYONGA LUDEWA AZIKWA
    Na Godlove Mtokambali
    Mheshimiwa diwani Rudolf Chaula ambaye alijinyonga ofisini kwake amezikwa jana tarehe 22/03/2012 katika makaburi ya kanisa katoliki kata ya mlangali. 
     
    Umati mkubwa sana ulifurika kumsindikiza marehemu katika makazi yake ya mwisho, ukiwemo uongozi wa wilaya ya Ludewa na madiwani wa kata mbali za Ludewa. 
     
    Inasadikika kwamba marehemu alijinyonga baada ya kudhukumiwa kiasi cha shilingi milioni 81.
     
    Mwendesha msiba alisoma kikaratasi alichokiacha marehemu ambacho kinadai kati ya shilingi milioni 81 alizodhulumiwa, milioni 41 zilikuwa ni mali ya SACCOS Mlangali na milioni 40 ni mali ya familia ya marehemu. 
     
    Uongozi wa kanisa katoliki uligoma katakata kuuombea mwili wa marehemu. 
     
    Marehemu alijinyonga usiku wa kuamkia majuzi katika mojawapo ya vyumba anavyotumia kama ofisi yake ya udiwani kwa kamba ya mbuzi.