For home theatre system solution

Friday, June 1, 2012

ADDY...MOTO WA BONGO FLAVOUR TOKA NJOMBE
Na: Kalmas Konzo
Najua utasema humfahamu...Basi ngoja nikufahamishe...Jamaa anaitwa ADDY aka BROTHER... Ni mwanamuziki mkali wa miondoko ya BONGO FLAVOUR toka mkoani NJOMBE... Mwanamuziki huyu amebarikiwa kipaji cha pekee ikiwa ni sambamba na sauti tamu ya pekee ambayo haichoshi kuisikiliza.




Ni miaka kadhaa sasa imepita toka nimfahamu ADDY. Kwa mara ya kwanza nilipokutana naye nilitambua fika kwamba kijana huyu atafika mbali sana katika tasnia hii ya kizazi kipya hapa nyumbani Tanzania.


Ana kila sababu ya kupewa pongezi za dhati kutokana na kazi nzuri anazozifanya. Ukibahatika kuzisikiliza kazi zake utanielewa ni nini ninachokizumgumzia.

Kwa sasa anakuja na albamu akiwa anatesa na video yake ya UA... Karibuni sana mumpokee

Wednesday, May 30, 2012

CHARLES TAYLOR AHUKUMIWA MIAKA 50 JELA KWA UHALIFU LIBERIA

Rais wa zamani nchini Liberia Charles Taylor amehukumiwa miaka 50 jela na makahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita.

Mwezi jana Taylor alipatikana na makosa ya kuwaunga mkono waasi nchini Sierra Leone katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka 1991 na 2002.

Upande wa mashtaka ulitaka kiongozi huyo wa zamani kusukumwa jela miaka 80. Charles Taylor amesisitiza hana hatia yeyote na anatarajiwa kukata rufaa.

Mwandishi wa BBC aliyeko The Hague Anna Holligan anasema rufaa dhidi ya hukumu hii huenda ikachukua miezi sita. Akitoa hukumu hiyo Jaji Richard Lussick amesema dhuluma zilizotekelezwa nchini Siera Leone zilikuwa za kinyama zaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya binadamu.

Mahakama maalum ya Kimataifa inayochunguza dhuluma za kivita nchini Sierra Leone ilimpata Taylor na hatia ya makosa 11 dhidi ya binadamu ikiwemo mauaji na ubakaji.

Taylor amekuwa Rais wa kwanza kuhukumiwa kwa makosa ya vita na Mahakama ya Kimataifa tangu kesi za Nuremurgs dhidi ya watawala wa Kinazi baada ya Vita Kuu ya Pili duniani.

Charles Taylor amelalamikia upande wa mashtaka kwa kuwatisha mashahidi katika kesi dhidi yake. Rais huyo wa zamani anatuhumiwa kwa kuwapa silaha waasi na kubadilishana na almasi.

Kesi dhidi ya kiongozi huyo wa zamani wa Liberia inasikilizwa The Hague kwa hofu kwamba kufanyika kwake Sierra Leone huenda kukazua vurugu katika kanda hiyo. Taylor anatarajiwa kutumikia kifungo chake nchini Uingereza.

Sunday, May 27, 2012


BREAKINGNEWS.....RAIA WA INDIA ADAIWA KUNYANYASA WANAWAKE IRINGA ANAMILIKI MAHABUSU BINAFSI ,POLISI WAMSAKA

Mwanamke Edna Panzi (47) akiwa mahabusu katika ofisi za b\Barc zinazomilikiwa na raia huyo wa India zipo eneo la Ilala mjini Iringa
Polisi wakimhoji mwanamke huyo akiwa katika mahabusu
Wananchi wakiwa wameizunguka ofisi hiyo ya Brac eneo la Ilala mjini Iringa

Naibu meya wa Manispaa ya Iringa Grevas Ndaki akiungana na wananchi wake kushuhudia unyanyasaji wa raia huyo wa India dhidi ya wanawake

Polisi wakiwa wamefanikiwa kumtoa mahabusu mwanamke huyo

JESHI la polisi mkoani Iringa linamsaka mkurugenzi wa taasisi ya mikopo ya Brac ambaye ni Raia wa India kwa tuhuma za kumnyanyasa kwa kumfungia katika mahabusu binafsi ofisini kwake mwanamke mmoja Edina Panzi (47) mkazi wa Ilala katika Manispaa ya Iringa akimdai kiasi cha shilingi 5800 .

Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Peter Kakamba alisema kuwa raia huyo wa India anasakwa na jeshi la polisi mkoani Iringa baada ya kumfungia katika mahabusu mwanamke huyo ambaye alikopeshwa fedha na taasisi yake hiyo ya Brac tawi la Ilala mjini Iringa.

Bila kumtaja jina raia huyo wa India ,kamanda Kakamba alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 11 jioni katika eneo la Ilala ambako zipo ofisi za taasisi hiyo ya Brac baada ya jeshi la polisi kupata taarifa kutoka kwa rai wema kuhusiana na mwanamke huyo kufungia katika mahabusu katika ofisi hiyo kabla ya polisi kufika kumfungulia mlango mwanamke huyo.

"Jeshi la polisi lilipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuhusuana na mwanamke huyo kufungia katika mahabusu hiyo kwa sababu ambavyo raia huyo wa India anazijua yeye na ndipo polisi walipofika na kufanikiwa kufungua mahabusu hiyo na kumtoa mwamamke huyo "

Kakamba alisema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikijishughulisha na utoaji wa mikopo kwa wanawake jambo ambalo si baya ila ubaya unakuja pale ambapo mkopeshaji huyo anajichukulia sheria mkononi kwa kutoa adhabu iliyo kinyume na sheria za nchi hii kwa kuwafungia mahabusu wakopaji wake.

Kwani alisema kuwa haipo sheria inayomruhusu mtu awaye yeyote yule ama taasisi ya ulinzi kumiliki mahabusu kwa kukamata watu na kuwafungia mahabusu kwani kufanya hivyo ni kosa na wanapatikana na tuhuma kama hizo wakikamatwa hufikishwa mahakamani.

Hivyo alisema kuwa jeshi la polisi linaendesha msako mkali wa kumsaka mkurugenzi huyo wa Brac ambaye ni rai wa India ili kufikishwa mahakamani .

Kwa upande wake mwanamke huyo anayedaiwa kufungiwa mahabusu alisema kuwa alifungiwa katika mahabusu hiyo juzi kuanzia majira ya saa 4 asubuhi hadi saa 11 jioni kabla ya waandishi wa habari wa mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) kuweza kufika eneo hilo na kutoa taarifa hiyo polisi .

Mwanamke huyo alisema kuwa jumla ya deni lote alilokopa lilikuwa ni kiasi cha shilingi 500,000 na hadi anakamatwa na kufungiwa katika mahabusu hiyo alikuwa akidaiwa kiasi cha shilingi 5800 pekee .

Diwani wa kata hiyo ya Ilala ambaye pia ni naibu meya wa Manispaa ya Iringa Grevas Ndaki alisema kuwa uongozi wa kata hiyo hauungi mkono hata kidogo unyanyasaji unaofanywa na Raia huyo wa India kwa wanawake wa kata hiyo na kuwa kutokana na tabia hiyo kuendelea kuchukua kasi wanaona ni vema ofisi hiyo kuondolewa katika kata hiyo .

ANASWA AKITUHUMIWA KUVUNJA NEEMA CRAFTS IRINGA

Kijana ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja mkazi wa kata ya Makorongoni mjini Iringa akiwa amewekwa chini ya ulinzi baada ya kukutwa akivunja eneo la ofisi za Neema Crafts mjini Iringa jana usiku (picha na Jeremia Chaula Photo wa www.blogspot.com)
Hapa akiadhibiwa kwa kumwagiwa maji ya baridi
Jamani wadau anafahamika huyo?
Vijana hawa wanadaiwa kuwa kundi la vijana zaidi ya wanne na baada ya kukurupushwa na walinzi walikimbia na kumsahau mwenzao huyo ambaye aliwekewa mtigo na walinzi wa eneo hilo ,nyuma yake ni eneo ambalo walianza kulivunja kulia

Sabodo atoa bilioni 5/- kujenga jengo la kuegesha magari


Na Dotto Mwaibale
 
MFANYABIASHARA maarufu nchini, Mustafa Sabodo ametoa zaidi ya sh.bilioni 5 kwa madhehebu ya Khoja Shia Ithnaashri Jamat kwa ajili ya kujenga jengo la maegesho ya magari.
Akizungumza katika hafla ya kupokea vibali vya ujenzi wa jengo hilo Dar es Salaam leo kutoka kwa Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa alisema jengo hilo litasimamiwa na madhehebu hayo.
Alisema jengo hilo lililopo katika mitaa ya India na Morogoro la ghorofa 14 litakuwa na uwezo wa kuhifadhi magari 180 kwa wakati mmoja.
Silaa alisema fedha zitakazopatikana kwa malipo ya maegesho ya magari katika kipindi cha miaka 10 zitafanya kazi ya kuchimba visima katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu.
Meya alisema kwa muda mrefu Jiji la Dar es Salaam limekuwa likikabiliwa na maeneo ya kuegesha magari na kuwa jengo hilo la kwanza kubwa litakuwa ni mkombozi mkubwa.
"Kwa muda mrefu tumekuwa na matatizo ya kuegesha magari katika jiji letu hivyo msaada aliotoa ndugu yetu Sabodo kwa madhehebu hayo ya ujenzi wa maegesho hayo itasaidia sana kupunguza tatizo hilo," alisema Silaa.
Alisema Manispaa imepokea jambo hilo kwa mikono miwili na ndio maana imekamilisha vibali ili ujenzi huo uende pasipo kikwazo chochote.
Alisema jengo hilo litaitwa Sabodo Car Park jambo litakalo weka kumbukumbu ya mchango wake katika kufanikisha shughuliza za maendeleo.
Mwenyekiti wa Madhehebu hayo Shiraz Walji, alimshukuru Sabodo kwa msaada wake huo na kuahidi kusimamia vizuri mradi huo ambao utakuwa wa manufaa kwa Watanzania wote.
 
Zanzibar yalipuka
Monday, 28 May 2012 08:21
Moto ukiwaka katikati ya mtaa mjini Zanzibar jana baada ya vurugu za wanaharakati kupinga muungano na kudai Zanzibar ijitawale. Picha na Salma Said
MAKANISA YACHOMWA, WABARA WATAKIWA KUONDOKA
Salma Said, Zanzibar
ZANZIBAR imechafuka. Baada ya kuwapo kwa amani kwa takribani mwaka mmoja tangu kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, vurugu na hali ya wasiwasi zimeibuka tena baada ya wanaharakati wa Kiislam kufanya maandamano kutaka uhuru wa visiwa hivyo.Zanzibar ilijikuta katika hali tete kiusalama tangu mwaka 1995 baadaya kutangazwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa Rais, ambayo Chama cha Mapinduzi (CCM) kiilibuka kidedea na Chama cha Wananchi (CUF) kupinga, lakini uhasama huo ulizikwa Julai 31 mwaka 2010, baada ya kura ya maoni ya kuunda Serikali hiyo ya umoja wa kitaifa.

Lakini kuanzia juzi usiku hadi jana jioni mji wa Unguja na viunga vyake ulitikiswa na mabomu ya kutoa machozi ambayo polisi waliyatumia kutawanya mamia ya wanaharakati hao wa Kiislam wakiongozwa na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI).

Mabomu ya machozi yalipigwa mfululizo juzi usiku na kuendelea kutwa nzima jana, hivyo kuathiri shughuli za biashara, ibada katika makanisa mbalimbali na kusababisha hofu kwa wananchi.

Kwa muda wa saa takriban mbili hivi kati ya saa 3:00 na saa 5:00 asubuhi, helkopta ya polisi ilikuwa ikipasua anga la Zanzibar ambalo lilikuwa limetandwa na moshi uliotokana na mabomu ya machozi pia uchomaji wa matairi ya magari. 
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa aliwaambia waandishi wa habari kuwa wafuasi hao wamefanya uharibifu mkubwa ikiwa pamoja na kuchoma moto makanisa mawili na kwamba, watu saba akiwamo Imamu wa Msikiti wa Bizeredi, Maalim Mussa Juma wanaotuhumiwa na matukio hayo wamekamatwa na jeshi hilo.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Kiongozi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Askofu Dickoson Maganga alisema watu wasiojulikana walivamia kanisa lao eneo la Kariakoo Mjini Zanzibar mnamo saa 4.30 usiku na kuvunja ukuta, kuchoma viti vya plasitiki pamoja na gari yake.

Chanzo cha vurugu hizo kinatajwa kuwa ni wanaharakati hao juzi kufanya mkusanyiko na maandamano makubwa ya kushtukiza ambayo yalizistua mamlaka za usalama visiwani humo, lakini baada ya kutawanyika jioni baadhi ya viongozi wa maandamano hayo walitiwa mbaroni.

Baada ya kukamatwa kwao, wafuasi wao walikusanyika makao makuu ya polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Madema, kushinikiza kutolewa kwa viongozi hao wanaoshikiliwa kituoni hapo.

Habari zaidi zinasema kutokana na hali ilivyo, askari polisi walitarajiwa kuongezwa visiwani humo, ili kusaidia kuimarisha hali ya usalama pia kuwadhibiti wahalifu ambao walikuwa wameanza kuelekea nje ya maeneo ya mji.

Tayari kuna taarifa kuwa askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kutoka Tanzania bara jana mchana walingia Zanzibar kwa ajili ya kuongeza ulizi katika mji wa Unguja.

Hata hivyo, katika hali ya kushangaza hakuna kiongozi yoyote wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) aliyetoa kauli kuhusu hali hiyo.

Kauli ya Polisi
Kamishna Mussa alisema jeshi lake litaendelea kuwasaka na kuwatia mikononi wote waliopanga fujo hizo pamoja na viongozi wote wa JUMIKI.

“Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar ndio iliyohusika na kuwachochea vijana kukusanyika na kufanya uharibifu ikiwemo kuchoma moto gari, kupanga mawe barabarani na kufanya hujuma mbalimbali kinyume cha sheria. Tutaendelea kuwasaka kwa gharama zote,” aliapa Kamishna Mussa.

Alifafanua kwamba kwa sasa mikusanyiko yote ya mihadhara ya kidini na vyama vya siasa, lazima ipate kibali cha polisi vyinginevyo jeshi lake litatumia nguvu za ziada kutawanya mikusanyiko hiyo ili kulinda sheria za nchi, amani na utulivu.

Hata hivyo, kamishna huyo wa polisi alijizuia kuhusisha harakati za Uamsho na chama cha siasa wala kutaja majina ya viongozi ambao tayari wanashikiliwa na jeshi lake.

“Mpaka sasa hivi sina majina yao kwa jumla, lakini tumewakamata viongozi wa Uamsho na tunatendelea kuwasaka lakini jina moja tu ndio ninalo ambalo ni Mussa Abdallah Juma,” alisema Kamishna huyo.

Hali bado tete
Wakati jeshi la polisi litoa onyo hilo, hali ya usalama ilionekana kuwa bado tete huku maeneo kadhaa ya Mji wa Zanzibar hasa Darajani na Michenzani ambako muda wote ni sehemu zenye harakati nyingi za biashara, jana zilikuwa zimebakia bila pilikapilika kutokana na askari waliojihami kufanya doria katika mitaa yote na kulipua mabomu kila penye kikundi cha watu waliokusanyika wakinywa kahawa.

Mitaa hiyo ilikuwa imechafuliwa kwa mawe, matofali na magogo yaliowekwa barabarani ili kuziba njia kwa ajili kuzuia magari yasipite huku mipira ya magari ikiwashwa moto na vijana hao.

Kwa upande wake Askofu Maganga akizungumzia uvamizi kisha uhalifu uliofanywa kanisani kwake alisema:
“Nasikitika sana kwa tukio hili ambalo tayari tumeiarifu polisi ambao jana (juzi), usiku walifika hapa wakishirikiana na kikosi cha kuzima moto na kufanikiwa kuuzima moto huo ambao kwa habati nzuri haujaathiri paa la kanisa letu,” alishukuru kiongozi huyo.

Alisema kundi la watu ambalo lilikuwa likitoa maneno ya kashfa na kutishia maisha ya waumini waliokuwa wakifanya ibada usiku huo, lilikatisha ibada hiyo pamoja na kusababisha uharibifu wa mali ya kanisa hilo yenye thamani ya zaidi ya Sh 100 millioni.

Kauli ya JUMIKI
Kutokana na hali hiyo, jumuiya hiyo jana ilitoa taarifa yake kwa vyombo vya habari ikikanusha kuhusika na kuchochea watu kuchoma kanisa wala kuharibu mali za watu.

Hata hivyo, Katibu wa Jumuiya hiyo, Abdallah Said alisema katika taarifa hiyo kwamba jeshi la polisi linapaswa kubeba lawama kwa yote yaliotokea kutokana na kuvunja sheria na kuwakamata viongozi bila ya utaratibu wa busara.

“Uislamu ni dini ya amani na inahimiza ushirikiano na utulivu na hatuwezi kuwatuma watu kwenda kuvunja makanisa na kuharibu mali, kwa sababu ndani ya imani zetu tunajua hilo ni kosa na jambo ambalo halifai katika maamrisho ya dini yetu,” alisema Sheikh Abdallah.

Taarifa hiyo ilisema pia kwamba jumuiya hiyo imekuwa wazi katika kudai maslahi ya Zanzibar na sio vinginevyo na kuahidi kufanya hivyo kwa njia za amani, na iwapo watakuwa wamekosea basi wapo tayari kufikishwa katika vyombo vya sheria.

“Ni lazima polisi wajue kwamba tupo tayari kufanya kazi kwa misingi ya kisheria na hata kwa kujisalimisha tupo tayari, lakini ukamataji bila kufuata busara na sheria haukubaliki. Tunachokitaka ni kura ya maoni haraka na hilo tutaendelea kulidai,” alisisitiza katibu huyo wa JUMIKI.

Wakati viongozi wa Uamsho wakiendelea kutafutwa na jeshi la polisi, nyumba ya kiongozi aliyeongoza maandamano juzi Sheikh Farid Hadi Ahmed inadaiwa kuvunjwa milango usiku wa manane alipokuwa akiswakwa jeshi hilo.

Hata hivyo, taarifa hizo hazikuthibitishwa iwapo ni polisi waliofanya kitendo hicho au la,  wanafamilia wanasema waligongewa milango na kutakiwa wafungue baada ya kutofungua walisikia kishindo kikubwa cha kusukumwa milango katika eneo la Mbuyuni Mjini Unguja.

Vijana katika mitaa ya Zanzibar jana walionekana wakiwa na hamasa kubwa wakidai kuendelea kuungana na viongozi wao kudai haki ya Zanzibar, pamoja na kutaka Zanzibar huru kutoka ndani ya mikono ya Muungano.

“Sisi tunachokitaka Zanzibar yetu watupige mabomu, watuue, watukamate lakini tunataka Zanzibar yetu na hatusikii lolote,” walisikika baadhi ya vijana.

Hada jana jioni vurugu katika badhi ya maeneo hususan Kwelekwe na njia ya Baa ya Amani zilikuwa zikiendelea na gari moja lilichomwa moto karibu na ofisi ya CCM.

Matukio kabla
Zanzibar imekuwa ikitawaliwa na matukio ya ghasia ambayo licha ya mihadhara hiyo ya Kiislam ilikuwa ni uhasama wa kisiasa kati ya vyama vikuu vya CUF na CCM, hatua ambayo iliwahi kusababisha mauaji ya Januari 27, mwaka 2001.

Lakini, uhasama huo wa kisiasa ambao ni wa kihistoria ulizikwa baada ya kura hiyo ya maoni na uchaguzi mkuu wa 2010 hatua ambayo imemfanya Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa SMZ huku baadhi ya mawaziri pia wakitoka katika chama hicho.

Hata hivyo, wanaharakati hao wa Kiislam wameanza upya kuilipua Zanzibar wakishinikiza visiwa hivyo viwe taifa huru kwa kujitenga katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Zitto ataka tume ya uchunguzi
Katika hatua nyingine Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amemtaka Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein aunde kikosi kazi maalum kwa ajili ya kudhibiti
vurugu hizo na kuanza mazungumzo na pande zote kwa kuwa, "Hiki sio kitendo cha kudharau
kabisa."

Alifafanua kwamba waliochoma nyumba za ibada wasakwe na kufikishwa mbele ya sheria mara
moja na kuongeza, "Tusiruhusu hata kidogo wapuuzi wachache kutuingiza katika vurugu za
kidini ili kufikia malengo yao ya kisiasa."