For home theatre system solution

Sunday, May 27, 2012


BREAKINGNEWS.....RAIA WA INDIA ADAIWA KUNYANYASA WANAWAKE IRINGA ANAMILIKI MAHABUSU BINAFSI ,POLISI WAMSAKA

Mwanamke Edna Panzi (47) akiwa mahabusu katika ofisi za b\Barc zinazomilikiwa na raia huyo wa India zipo eneo la Ilala mjini Iringa
Polisi wakimhoji mwanamke huyo akiwa katika mahabusu
Wananchi wakiwa wameizunguka ofisi hiyo ya Brac eneo la Ilala mjini Iringa

Naibu meya wa Manispaa ya Iringa Grevas Ndaki akiungana na wananchi wake kushuhudia unyanyasaji wa raia huyo wa India dhidi ya wanawake

Polisi wakiwa wamefanikiwa kumtoa mahabusu mwanamke huyo

JESHI la polisi mkoani Iringa linamsaka mkurugenzi wa taasisi ya mikopo ya Brac ambaye ni Raia wa India kwa tuhuma za kumnyanyasa kwa kumfungia katika mahabusu binafsi ofisini kwake mwanamke mmoja Edina Panzi (47) mkazi wa Ilala katika Manispaa ya Iringa akimdai kiasi cha shilingi 5800 .

Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Peter Kakamba alisema kuwa raia huyo wa India anasakwa na jeshi la polisi mkoani Iringa baada ya kumfungia katika mahabusu mwanamke huyo ambaye alikopeshwa fedha na taasisi yake hiyo ya Brac tawi la Ilala mjini Iringa.

Bila kumtaja jina raia huyo wa India ,kamanda Kakamba alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 11 jioni katika eneo la Ilala ambako zipo ofisi za taasisi hiyo ya Brac baada ya jeshi la polisi kupata taarifa kutoka kwa rai wema kuhusiana na mwanamke huyo kufungia katika mahabusu katika ofisi hiyo kabla ya polisi kufika kumfungulia mlango mwanamke huyo.

"Jeshi la polisi lilipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuhusuana na mwanamke huyo kufungia katika mahabusu hiyo kwa sababu ambavyo raia huyo wa India anazijua yeye na ndipo polisi walipofika na kufanikiwa kufungua mahabusu hiyo na kumtoa mwamamke huyo "

Kakamba alisema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikijishughulisha na utoaji wa mikopo kwa wanawake jambo ambalo si baya ila ubaya unakuja pale ambapo mkopeshaji huyo anajichukulia sheria mkononi kwa kutoa adhabu iliyo kinyume na sheria za nchi hii kwa kuwafungia mahabusu wakopaji wake.

Kwani alisema kuwa haipo sheria inayomruhusu mtu awaye yeyote yule ama taasisi ya ulinzi kumiliki mahabusu kwa kukamata watu na kuwafungia mahabusu kwani kufanya hivyo ni kosa na wanapatikana na tuhuma kama hizo wakikamatwa hufikishwa mahakamani.

Hivyo alisema kuwa jeshi la polisi linaendesha msako mkali wa kumsaka mkurugenzi huyo wa Brac ambaye ni rai wa India ili kufikishwa mahakamani .

Kwa upande wake mwanamke huyo anayedaiwa kufungiwa mahabusu alisema kuwa alifungiwa katika mahabusu hiyo juzi kuanzia majira ya saa 4 asubuhi hadi saa 11 jioni kabla ya waandishi wa habari wa mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) kuweza kufika eneo hilo na kutoa taarifa hiyo polisi .

Mwanamke huyo alisema kuwa jumla ya deni lote alilokopa lilikuwa ni kiasi cha shilingi 500,000 na hadi anakamatwa na kufungiwa katika mahabusu hiyo alikuwa akidaiwa kiasi cha shilingi 5800 pekee .

Diwani wa kata hiyo ya Ilala ambaye pia ni naibu meya wa Manispaa ya Iringa Grevas Ndaki alisema kuwa uongozi wa kata hiyo hauungi mkono hata kidogo unyanyasaji unaofanywa na Raia huyo wa India kwa wanawake wa kata hiyo na kuwa kutokana na tabia hiyo kuendelea kuchukua kasi wanaona ni vema ofisi hiyo kuondolewa katika kata hiyo .

No comments:

Post a Comment