For home theatre system solution

Friday, March 16, 2012

DAR ES SALAAM

WAKUU WA MIKOA MIPYA MINNE WATANGAZWA
Na Sandahillary Mnyawusuha
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete,
    amewateua wafuatao kuwa Wakuu wa Mikoa .

    Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa KATAVI . Kabla ya hapo Dkt. Rutengwe alikuwa Mkuu wa wilaya ya Mpanda.

    Ndugu Magalula Saidi Magagula ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa GEITA . Kabla ya hapo Ndugu MAGALULA alikuwa Mkuu wa wilaya ya Lindi.

    Ndugu Paschal Kulwa Mabiti ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa SIMIYU . Kabla ya hapo Ndugu MABITI alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Singida.

    Kapt. Asery Msangi ameteuliwa kuwa Mkuu wa
    Mkoa wa NJOMBE . Kabla ya hapo Kapt. MSANGI alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa.

    Uteuzi huu unaanza tarehe 15 Machi, 2012 . Wataapishwa Ikulu, Dar es Salaam, Jumatano tarehe 21 Machi, 2012 saa 04:00 asubuhi .

    Imetolewa na : Kurugenzi ya Mawasiliano ya
    Rais, Ikulu . Dar es Salaam. 15 Machi, 2012