For home theatre system solution

Friday, February 17, 2012

STEVE WONDER, ARETHA FLANKLIN KUTUMBUIZA MAZISHI YA WHITNEY HOUSTON

NEW JERSEY, Marekani


WAIMBAJI Aretha Franklin na Stevie Wonder wanatarajiwa kuimba kwenye maziko ya mwimbaji, Whitney Houston anayetarajiwa kuzikwa kesho jirani na kanisa alilokuwa akiimbia utotoni New Hope Baptist la Newark.
Mwimbaji Kristen Foster pia amethibitisha kushiriki kuimba katika maziko hayo akiwa amepewa mualiko na mume wa zamani wa Houston, Bobby Brown.

Wengine wataoshiriki ni mwanamuziki nguli, Clive Davis, anatarajiwa kuzungumza katika maziko hayo, mwimbaji wa injili na rafiki mkubwa wa familia Marvin Winans.

Wengine wanaotarajiwa kushiriki katika maziko hayo ni Donnie McClurkin, Tyler Perry, Kim Burrell, Rickey Minor, Alicia Keys, Dionne Warwick na Cece Winans, Foster na wengineo.

Houston alifariki jumamosi jijini Beverly Hills, California akiwa na umri wa miaka 48.
Chanzo: mamapipiro.blogspot.com

MSANII SIMON MWAPAGATA ‘RADO’ ATOA MSAADA KWA WATOTO VIZIWI BUGURUNI KWA KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI YA STEPS ENTERTAINMENT.


Msanii wa filamu nchini Simoni Mwapagata (Rado) (kushoto) akitoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo Juice na Biskuti kwa mtoto wa shule ya Buguruni Viziwi,Isack Ntira jijini Dar es salaam. Msaada huo umetolewa na msanii huyo kwa kushirikiana na kampuni ya Steps Entertainment kulia ni Ibrahim Mbena.(Picha na www.burudan.blogspot.com).
Sitta matatani
Waziri wa Afrika Mashariki,Samuel Sitta

Na Festo Polea  Global Publishers Ltd
WAZIRI wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ameingia matatani baada ya Jeshi la Polisi nchini kutolea tamko ugonjwa wa Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe na kueleza kuwa hautokani na kulishwa sumu, huku likisema limefungua jalada kwa ajili ya uchunguzi wa kauli yake hiyo.

Tamko hilo la polisi lililotolewa jana na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Manumba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.  DCI Manumba aliwataka watu kuupuza madai hayo akieleza kuwa ushahidi uliopatikana kutoka nchini India alikolazwa Dk Mwakyembe hauonyeshi kuwa alilishwa sumu.  Manumba alitoa kauli hiyo alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam muda mfupi baada ya kumaliza mkutano wake kuhusu hali na mwenendo wa uhalifu nchini katika kipindi cha mwaka jana.

Akifafanua kuhusu kauli hiyo ya Waziri Sitta, DCI Manumba alisema, "Jeshi la Polisi limekaa kimya muda mrefu likifanyia uchunguzi kauli hiyo kwa kuwa maneno hayo ndani yake yanaonyesha jinai."  Aliendelea “Kazi ya Jeshi la Polisi ni kuchunguza makosa na si kufuatilia nani anaumwa ugonjwa gani. Nani anaumwa nini ni jukumu la madaktari. Lakini tumekuwa kimya muda mrefu tukichunguza tuhuma hizo nzito.’’  DCI Manumba aliendelea kufafanua “Ukweli kuhusu kauli hiyo inayodai kuwekewa sumu, tumeupata baada ya kuwasiliana na Wizara ya Afya ambayo nayo imewasiliana na hospitali aliyokuwa amelazwa Dk Mwakyembe nchini India.

Taarifa zinaonyesha kuwa hakuna sumu katika maradhi yanayomsibu Mwakyembe.’’   Manumba aliongeza kuwa kwa kuwa suala hilo ni la kisheria na kiupelelezi, Jeshi la Polisi linaandaa jalada la upelelezi kuhusu kauli hiyo ya Waziri Sitta na likikamilika, litapelekwa kwa DPP kwa ajili ya uamuzi.

“Hata hivyo, Sitta mwenyewe nilimsikia katika kauli yake akisema kuwa naye ameisikia katika vyombo vya dola, hivyo tunaandaa jalada la upelelezi na likikamilika litapelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka kwa uamuazi wa kisheria wa nani ashtakiwe au nani ana makosa. Lakini sasa ni hayo kuhusu kauli hiyo Waziri Sitta ninayoweza kusema,’’ alisema Manumba.

Awali Manumba alisema kabla Dk Mwakyembe hajaanza kuumwa na kukimbizwa India kwa matibabu, Jeshi la Polisi lilipokea maandishi kutoka kwa waziri huyo yaliyodai kuwa alikuwa akitishiwa uhai wake, lakini likiwa katika hatua za mwisho kukamilisha upelelezi wake, akaanza kuugua na kukimbizwa India kwa matibabu.

“Jeshi la Polisi liliwahi kupata maandishi kutoka kwa Mwakyembe kuwa anatishiwa uhai wake, lakini tukiwa katika hatua za mwisho za uchunguzi, Mwakyembe akaanza kuumwa,’’ alisema Manumba.   Historia ya ugonjwa wa Mwakyembe  Dk Mwakymbe alianza kuumwa Oktoba 9 mwaka jana na baadaye kupelekwa nchini India na kulazwa katika Hospitali ya Apollo kwa matatibu. Alirejea nchini Desemba 11, mwaka jana baada ya kulazwa hospitalini  humo kwa takribani miezi miwili.

Msemaji wa familia ya Dk Mwekyembe na Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa alisema mara baada ya mbunge huyo wa Kyela kurudi nchini kuwa, afya yake ni nzuri ndio maana ameruhusiwa kutoka hospitali.

 Kauli za Waziri Sitta   Mara kadhaa Waziri Sitta amekuwa akinukuliwa na vyombo vya habari akisisitiza kuwa ugonjwa wa Dk Mwakyembe, umetokana na kulishwa sumu.  Akiwa kwenye uzinduzi wa Programu ya Neno la Hekima kutoka kwa Kiongozi iliyoanzishwa na Kanisa la Ufufuo na Uzima la Kawe, Jijini Dar es Salaam Januari 28 mwaka huu, Sitta alisema:

“ Nasema Dk Mwakyembe kapewa sumu, kama vyombo vya uchunguzi vinasema siyo, basi watueleze ukweli, tena haraka,” alisisitiza Waziri Sitta katika hafla hiyo.

Sitta alihoji “ Ni vipi uone binadamu ambaye ukimshika katika ngozi unga unamwagika chini, mhudumu anakuja kuufagia, lakini baada ya saa moja unarudia tena, kitu hicho si cha kawaida.”   Sitta alisema wamejaribu wameshindwa kwa kuwa Dk Mwakyembe analindwa kwa jina la Yesu ambalo ni kubwa kuliko yote.

Waziri Nahodha
 Akijibu moja ya kauli hizo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nohodha alimtaka Waziri Sitta awasilishe ushahidi wake ili ufanyiwe kazi badala ya kuzungumza nje ya vyombo vya sharia.  Hata hivyo, Sitta alisema hatapeleka ushahidi wa madai aliyotoa kuwa Dk Mwakyembe alilishwa sumu kwa kuwa polisi tayari wanao ushahidi.

Alisema wanachotakiwa kufanya Polisi ni kufanya uchunguzi kuhusu madai hayo ya Dk Mwakyembe kulishwa sumu kwa kuwa ushahidi wanao na wasianze kurushiana mpira.
“Waziri Nahodha anataka ushahidi gani ikiwa taarifa za madaktari zinazomhusu Dk Mwakyembe kuhusu sumu aliyopewa  zilishapelekwa polisi, anataka mimi nitoe ushahidi gani,” alisema Waziri Sitta.

Kuhusu mwenendo wa uhalifu nchini kipindi cha kuanzia Januari hadi Desemba mwaka jana 2010, Manumba alisema kulikuwa na matishio mbalimbali ya usalama ikiwamo ugaidi, uharamia baharini, wahamiaji haramu na biashara haramu ya usafirishaji binadamu.  Manumba alitaja matishio mengine yaliyojitokeza mwaka huo kuwa ni uingizwaji bidhaa bandia na silaha haramu, dawa za kulevya, migogoro ya kisiasa, kidini, migogoro ya wanafunzi wa taasisi na vyuo vya elimu ya juu na migogoro na migomo ya wafanyakazi.  

DAR ES SALAAM

BASI LA ABOOD LAPATA AJALI ASUBUHI YA LEO MAENEO YA MBEZI

Basi la kampuni ya Abood likiwa limepinduka maeneo ya Mbezi wakati likitoka Mkoani Morogoro kuelekea Dar es salaam asubuhi ya leo.

Chanzo cha ajali hii hakikuweza kufahamika mapema. Kwa mujibu wa walioshuhudia ajali hiyo wameeleza kuwa gari hilo lilikuwa likijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake.
Picha na Lukaza
Habari ni kwa hisani ya latestnews.blogspot.com

UJERUMANI

Rais Wulff wa Ujerumani ajiuzulu

Rais Christian Wulff akitoa tangazo la kujiuzulu
Rais wa Ujerumani Christian Wulff amejiuzulu. Kiongozi huyo amekuwa akikabiliwa na kashfa ya kupokea mkopo wa fedha katika njia ambazo si halali, na uungwaji mkono kwake umeshuka sana.
Katika hotuba yake muda mfupi uliopita, Christian Wulff ameshukuru kwa muda aliokaa madarakani kama Rais wa Ujerumani, akaongeza lakini kwamba ofisi hiyo kwa sasa inahitaji mtu mwenye hadhi bora na anayeaminiwa na wananchi. Amesema kwa sasa yeye hana hadhi hiyo.
Tangazo lake la kujiuzulu limekuja saa chache baada ya Mwendeshamashtaka mkuu kusema anaazimia kuomba kinga ya bwana Rais Wulff iondolewe ili uchunguzi ufanywe juu ya shutuma zinazomkabili.
Kuondolewa Kinga
Habari kwamba mwendeshamashtaka mkuu wa Serikali alikuwa ameomba kinga ya Rais iondolewe ili aweze kuchunguzwa imekuwa kama mlipuko wa bomu katika mji mkuu wa Ujerumani Berlin. Mwendeshamashtaka mkuuu alikuwa amesema kuwa uchunguzi wa makini umedhihirika kwamba kuna vigezo vya kutosha na vya kuaminika, kuonyesha kwamba Rais Christian Wulff alitumia vibaya madaraka yake alipokuwa waziri mkuu wa jimbo la Lower Saxony
Utaratibu wa kufanya hivyo unaeleweka; Mwendeshamshtaka mkuu humwandikia barua waziri wa sheria kuomba kinga hiyo iondolewe, na waziri huwasilisha barua hiyo bungeni. Baada ya ombi hilo kuwasili bungeni, Rais wa Bunge, Norbert Lammert anawajibika kuiarifu kamati ya kinga bungeni. Kamati hiyo hukutana na kutafakari ombi hilo na kisha kutoa mapendekezo yao mbele ya kikao cha bunge zima.
Kupoteza imani ya wanasiasa
Hadi sasa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amekuwa akiunga mkono uamuzi wa Rais Wulff kukataa kujiuzulu. Lakini shinikizo limekuwa likikua kutoka pande mbali mbali kumtaka Merkel kubadili mawazo yake.
Katika tamko lake kufuatia azma ya mwendeshamashataka mkuu kutaka kinga ya Rais Wulff iondolewe, chama kikuu cha upinzani cha Social Democrats, SPD, kiliunga mkono azma hiyo. Katibu Mkuu wa chama hicho Andrea Nahles amesema ni lazima Christian Wulff aondoke kwenye ofisi ya Rais.
''Tumekwishatamka wazi juu ya matukio haya kwamba lazima Rais Wulff ajiuzulu, na tumependekeza kwa Kansela Angela Merkel juu ya kumtafuta mtu mwingine wa kuchukua wadhifa wa Urais bila kujali anatoka chama gani cha kisiasa. Kwa sasa jambo hilo ni muhimu kulioko wakati wowote ule mwingine.'' Andrea Nahles alisema.
Chama cha Kijani na Chama cha mrengo wa kushoto vimetangaza misimamo inayofanana na huo wa SPD, kwamba bwana Wulff hana hadhi tena ya kuendelea kutumikia ofisi.
Kwa zaidi ya miezi miwili iliyopita, Rais Wulff amekabiliwa na shutuma kashfa nyingi, zikiwemo kupokea mkopo kutoka kwa mfanyabiashara tajiri, na kujaribu kunyamazisha vyombo vya habari visizungumzie kashfa zake. Hadi sasa alikuwa hajaonyesha nia ya kujiuzulu, na ingawa kufukuzwa madarakani ni jambo linalowezekana, kuna vizingiti vingi vya kisiasa kufanya hivyo.
Katika hali inayoashiria kuwa maji yamefika shingoni katika kashfa hii inayomhusu Rais Christian Wulff, Kansela Angela Merkel ameahirisha kwenye dakika ya mwisho asubuhi ya leo, safari yake kwenda Italia kufanya mazungumzo na waziri mkuu wa nchi hiyo Mario Monti.

DAR ES SALAAM

Bifu la Isha Mashauzi, Rahma ni noma

Posted by GLOBAL on February 17, 2012 at 9:30am 3 Comments


Na Rhobi Chacha

Bifu kati ya Mkurugenzi wa kundi la muziki wa mwambao la Mashauzi Classic Morden Taarab, Aisha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’ (pichani) na muimbaji wa Jahazi Modern Taarab, Rahma Machupa ni noma kutokana na madai eti Rahma anadaiwa na Isha kuwa ‘anabinjuka’ na Thabit Abdul ‘Baby.’

Kwa mujibu wa chanzo chetu kilicho ndani ya kundi hilo, tuhuma za wawili hao kupeana ‘mambo’ zipo kitambo.

Kufuatia madai hayo, mwandishi wetu alimtafuta Rahma na kufanya naye mahojiano ambapo alifunguka:

“Kwanza napenda ieleweke kuwa nimejitoa Mashauzi Classic na…


Na Rhobi Chacha
Bifu kati ya Mkurugenzi wa kundi la muziki wa mwambao la Mashauzi Classic Morden Taarab, Aisha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’ (pichani) na muimbaji wa Jahazi Modern Taarab, Rahma Machupa ni noma kutokana na madai eti Rahma anadaiwa na Isha kuwa ‘anabinjuka’ na Thabit Abdul ‘Baby.’
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilicho ndani ya kundi hilo, tuhuma za wawili hao kupeana ‘mambo’ zipo kitambo.
Kufuatia madai hayo, mwandishi wetu alimtafuta Rahma na kufanya naye mahojiano ambapo alifunguka:
“Kwanza napenda ieleweke kuwa nimejitoa Mashauzi Classic na kuhamia Jahazi Modern Taarab, sababu kubwa ni maneno ya Isha kunishutumu kuwa natoka kimapenzi na Thabiti,” alisema msanii huyo.
Mashauzi aliposomewa mashtaka yake kuhusu madai hayo alisema hayana ukweli wowote.
“Unajua ukubwa ni jalala, hakuna kitu kama hicho, huyo Rahma anasema uongo tu labda anajua akiongea hivyo atapata umaarufu mapema kumbe anajiharibia,” alisema Isha.
Thabiti anayetuhumiwa kuchangia kuwepo kwa bifu kati wadada hao alipotafutwa alisema, yeye anatuhumiwa tu ila ukweli ni kwamba hana uhusiano na Rahma wala Isha kama inavyodaiwa.