For home theatre system solution

Friday, April 6, 2012

BREAKING NEWSzzzzzzzzzzzzz MSANII KANUMBA HAYUPO TENA DUNIANI


Msanii nyota wa filamu nchini Steven Kanumba pichani amefariki dunia eneo la Mbangala baada ya kupata ajali ya gari .

Imeelezwa kuwa msanii huyo alipata ajali hiyo wakati akitokea kwenye ukumbi wa burudani wa Dar Live usiku majira ya saa 7

Zipo tetesi kuwa Kanumba katika gari hilo alikuwa na mmoja kati ya warembo hapa nchini ambaye anadaiwa kuhusika katika kifo chake.

Mwili wa msanii huyo umehifadhiwa katika chumba cha maiti katikaHospital ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam na habari zaidi utaendelea kuzipata katika mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com .

Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake na lihimidiwe milele Amina .

RAIS WA MALAWI BINGU MUTHARIKA AFARIKI DUNIA

Aliyekuwa Rais wa Malawi, Bingu wa Mutharika enzi za uhai wake.

RAIS wa Malawi, Bingu wa Mutharika, amefariki baada ya shambulio la moyo, vyanzo vya hospitali na serikali ya nchi hiyo vilisema.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 78 alikimbizwa hospitali ya Lilongwe siku ya Alhamisi baada ya kuanguka na alitangazwa kuwa amefariki baada ya kufikishwa hapo.

Vyombo vya habari vya serikali vilisema alikuwa amepelekwa Afrika Kusini kwa matibabu japokuwa hakuweza kufahamika mara moja kabla ya hapo alikuwa wapi.

Wananchi wengi wa Malawi wamekuwa wakiulaumu utawala wa kiongozi huyo ambaye aliwahi kuwa mchumi wa Benki ya Dunia kwa matatizo ya kiuchumi ambayo yameikumba nchi hiyo.

“Tunajua amekufa na bahati mbaya amefia katika hospitali moja ndogo, miongoni mwa hospitali ambazo alikuwa hazijali, kwani zilikuwa hazina madawa ama umeme,” alisema Chimwemwe Phiri, mfanyabiashara wa mjini Lilongwe mmoja wa wananchi wengi waliofurahia kifo chake.

Katiba ya nchi hiyo inasema Makamu wa Rais, Joyce Banda, atakuwa mkuu wa nchi hiyo japokuwa alifukuzwa katika chama tawala cha DPP cha Mutharika mwaka 2010 kuhusiana na suala la kuchukua madaraka pindi rais anapofariki au kutoweza kuendelea kutawala.