Baraza la Mawaziri la Tanzania kuvunjwa?
Kamati
Kuu iliyokutana leo tarehe 27/04/2012 chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Dr.
Jakaya Mrisho Kikwete Jijini Dar es salaam, pamoja na mambo mengine
imefanya yafuatayo.;
A. UTEUZI
Kamati Kuu imeteua wafuatao kuwa makaimu Katibu wa mikoa. Vituo vyao vya
kazi vitapangwa baadae. Uteuzi huu unatokana na kuwepo kwa mikoa wazi
mitano, mikoa hiyo ni;
Geita
Njombe
Simiyu
Katavi
Magharibi
Hivyo wafuatao wameteuliwa kuwa makaimu katibu wa CCM wa Mikoa.
1. Ndg. Hilda Kapaya
2. Ndg. Shaibu Akwilombe
3. Ndg. Hosea Mpangile
4. Ndg. Alphonce Kinamhala
5. Ndg. Aziz Ramadhani Mapuri
B. HALI YA KISIASA:
Rais amepokea taarifa na maazimio ya Kamati ya wabunge wa CCM na Kamati
ya uongozi ya wabunge wa CCM juu ya kilichotokea kwenye bunge lililopita
mjini Dodoma.
Taarifa hizo zimewasilishwa kwenye kamati kuu na kujadiliwa. Pamoja na
taarifa hizo kamati Kuu imepokea taarifa ya jinsi Rais alivyojipanga
kuchukua hatua za kuwawajibisha mawaziri na watendaji wa serikali na
wale wa mashirika ya umma waliobainika kuhusika na ubadhirifu
ulioinishwa na taarifa ya Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za
Serikali, Kamati za kudumu za bunge na wabunge bungeni.
Kamati Kuu imeamua yafuatayo;
1. Kamati Kuu inatambua na kuheshimu haki na wajibu wa wabunge kujadili
utendaji wa serikali yao.Inapongeza juhudi za serikali kuhakikisha kuwa
ripoti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali inajadiliwa kwa
uwazi na hivyo kuibua mapungufu yaliyojadiliwa.
2. Kamati Kuu imeridhika na imebariki uamuzi wa Rais KULISUKA UPYA
BARAZA LA MAWAZIRI na taasisi zingine zilizoanishwa katika ripoti hizo.
Imesisitiza utekelezaji wa uamuzi huo ufanywe mapema iwezekanavyo.
Aidha kamati Kuu imeipongeza Kamati Teule ya baraza la wawakilishi
Zanzibar iliyoundwa kuchunguza utendaji katika sekta mbalimbali kwenye
serikali ya mapinduzi Zanzibar kwa taarifa yao.
Kamati Kuu inawapongeza wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa jinsi
walivyojadili taarifa hiyo na pia Kamati Kuu inaipongeza Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar kwa kuipokea taarifa na kuanza kuifanyia kazi.
Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
The Ideology and Publicity Secretary
Chanzo: Jamii forum