Waziri wa maliasili na utalii Mhe. Ezekiel Maige ameingiwa na hofu juu ya ujenzi wa nyumba mbili katika eneo la Wanging'ombe Wilaya ya Wanging'ombe mkoa wa Njombe baada ya kutembezwa kutazama nyumba hizo bila kusomewa taarifa ya mradi mzima .
Waziri Maige ambaye ametembelea ujenzi wa nyumba hizo jioni hii ameonyesha wasiwasi wake wa kubebeshwa maji katika tenga ( kudanganywa ) baada ya kukagua nyumba hizo ambazo mradi wake ulianzwa kutekelezwa mwaka 2004 bila ya kukamilika hadi sasa.
Baada ya kukagua mradi huo waziri Maige aliomba kusomewa taarifa ya mradi huo bila mafanikio zaidi msimamizi wa mradi huo ambaye ni meneja wa pori la akiba la mpanga Kipengele Bw.Benison Kibonde kudai kuwa taarifa ya mradi huo ameisahau ofisini kwake.
Kutokana na kukosekana kwa taarifa rasimi ya ujenzi huo jopo la wanahabari lilimvaa waziri huyo na kuomba kusaidiwa kupewa taarifa hiyo bila mafanikio zaidi ya meneja wa mradi huo kuishia kuomba kupewa mud a wa kutafuta taarifa hiyo.
Wanahabari hao walifikia hatua ya kuhoji zaidi juu ya ujenzi huo baada ya kuona sehemu ya jengo hilo likivunjwa jambo ambalo waliomba kuonyeshwa BOQ ya ujenzi huo na kujua gharama za marekebisho ya majengo hayo inatoka katika mfuko gani wakati tayari serikali ilitenga bajeti husika.
Kutokana na maswali hayo ya wanahabari meneja wa mradi huo alimweleza waziri kuwa gharama za ukarabati wa majengo hayo inachukuliwa na mkandarasi husika .
Akitolea ufafanuzi juu ya hoja za wanahabari hao waziri Maige alisema kuwa maswali ya wanahabari hao yamemgusa na hivyo kumwagiza meneja wa mradi huo kuhakikisha anawasilisha taarifa hiyo Leo kabla ya kuondoka mkoani Njombe Kwenda mkoa wa IRINGA .
wakati huo huo watumishi wa idara hiyo wameeleza changamoto mbali mbali zinazowakabili zikiwemo za kutojua mipaka ya hifadhi hiyo kutokana na mwingiliano uliopo Kati ya wananchi na eneo la hifadhi.
Pia suala la Kupanda kwa mishahara yao huku wakimpongeza meneja wao Benison Kibonde kwa kazi nzuri ya kusimamia ofisi hiyo kutokana na meneja aliyekuwepo Awali kutokuwa na mahusiano mazuri na watumishi wenzake.
wakati huo huo waziri Maige amesema kuwa meneja huyo hajamtendea haki kutokana na kushindwa kutoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa nyumba pamoja na taarifa nzima ya ofisi yake na kuwa kutofanya hivyo ni kutomtendea haki.
"Kwa kweli kupewa taarifa ya mdomo bila kusomewa wala kupewa nakala ya taarifa husika ni kutonitendea haki Kwani taarifa Ndio inanifanya kuweza kujua zaidi na Kwenda kuitendea kazi.....sasa kushindwa kunipa taarifa ni kutonitendea haki Kabisa ...japo nimeagiza kupewa taarifa hiyo nikiwa Makambako ila bado ni kutonitendea haki kutokana na wakati huo Mimi ni wakati wa kupumzika"
Katika hatua nyingine Waziri Maige amewataka askari hao kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na sheri a badala ya kuendelea kuwabambikizia wananchi makos a ili kuomba Rushwa .
Waziri Maige amewataka askari hao kuepuka kutumia nguvu kwa kuwakamata wananchi na kuwa ofisi yake haitahusika na askari wanaoshindwa kufuata sheri a na kuwa wapo askari wanaochinjwa kutokana na unyama ambao wamekuwa wakiufanya kwa wananchi.
Chanzo: francisgodwin.blogspot