For home theatre system solution

Monday, March 19, 2012

DIWANI WA CCM LUDEWA AJINYONGA USIKU HUU

Marehemu Rudolph Chaula a.k.a Kacheche kushoto

Chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Ludewa mkoa mpya wa Njombe kimepata pigo kubwa kufuatia diwani wake wa kata ya Mlangali Rudolph Chaula maaarufu kwa jina la Kacheche kujinyonga .

Taarifa ambazo mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com umezipata hivi na kuthibitishwa na katibu wa CCM wilaya ya Ludewa Eva Degeleki zinadai kuwa diwani huyo amekutwa akiwa kajinyonga katika moja kati ya vyumba vya nyumba yake ambavyo katika enzi ya uhai wake alikuwa akitumia kama ofisi yake ya udiwani.

Katibu huyo wa CCM Ludewa amesema kuwa hadi sasa hana taarifa za chanzo cha kifo chake ila anataarifa ya kujinyonga kwa diwani huyo na kuwa amepokea taarifa hiyo mida ya saa 8.15 usiku huu kujulishwa juu ya kifo hicho.


Imedaiwa kuwa diwani huyo toka mida ya mchana familia yake ilikuwa ikimsaka bila mafanikio baada ya wageni kufika kumuulizia na jitihada za kutafuta huku na kule zilimezao matunda usiku huu baada ya kuwa na wazo la kuvunja chumba hicho na kumkuta diwani huyo akiwa kajinyonga.
 

Habari kwa hisani ya: www.francisgodwin.blogspot.com 

No comments:

Post a Comment