For home theatre system solution

Monday, February 13, 2012

NA Gladness Mallya
NYOTA wa sinema za Kibongo, Rose Donatus Ndauka ameruka kimanga madai kwamba, amebadili dini kwa sababu ya kufuata ndoa, Risasi Jumamosi lina sauti yake mkononi.
Akizungumza juzikati jijini Dar es Salaam, Rose ambaye sasa anaamini katika Uislam alisema amefuata dini ya mama yake mzazi na si vinginevyo.
“Sijabadili dini ili niolewe na mwanaume wa Kiislam ila ni kwa sababu mama yangu mzazi ni Muislam.
“Nilitaka kufanya hivyo siku nyingi lakini sasa naona ni muda muafaka ili niwe sambamba na mzazi wangu,” alisema staa huyo wa filamu ya Mahabuba.
Kauli za wadau wa filamu za Bongo kudai msanii huyo alibadili dini na sasa anaitwa Aisha lengo awe sare kwenye ndoa, zilitolewa mara baada ya Rose kuposwa na Marik Bandawe  ‘Chiwa’ ambaye ni Muislam.
Rose anatarajia kufunga ndoa mapema mwezi Mei, 2012 baada ya kufanyiwa Kitchen Party na Send Off ya nguvu mwezi Aprili, jijini Dar es Salaam.

AY, MWANA FA, CHEGGE, TEMBA, DOGO ASLAY WAFANYA ‘KURUFU’ DAR LIVE

AY (kushoto) na Mwana FA wakikamua.
...Wakiendelea kuwapagawisha mashabiki.
Temba akichana mistari.
Chegge (kushoto) na Temba wakiwika stejini.
...Wakiuimbisha umati kituoni hapo.
Mwanamuziki  Shilole naye alikuwepo.
Dogo Asley akifanya vitu vyake.
...Akionyesha hazina yake ilivyo.
Mwanamuziki wa  'Twanga Pepeta', Luiza Mbutu (kushoto), akiimba na kucheza.
Msafiri Diouf akiwapa raha mashabiki.
Wanenguaji wa Twanga Pepeta wakionyesha ‘matindo’.
...Wakitoa staili ya ‘tufe pamoja’.
Zamu ya Wakali Dancers.
Mmoja wa washiriki wa ‘Vaa, Imba, Cheza Kama Rihanna’ akijinafasi.
Kina ‘Rihanna’ wakiwa pamoja.
East African Melody wakiwa kazini.
Afua Selemani wa East African Melody.
Mashabiki lukuki walioijaza Dar Live.
KITUO cha maraha cha Dar Live kilichoko Mbagala jijini Dar kilirindima kwa vifijo vya burudani ya muziki  kutoka vikundi mbalimbali vya wasanii.

Ilikuwa ni ‘kufuru tupu’ wakati wasanii AY akishirikiana na Mwana FA walipotoana jasho na wenzao kina  Chegge na Temba kutoka katika kundi la Wanaume Family yote hayo yakisindikizwa na burudani kutoka kundi la taarabu la East Africa Melody, Wakali Dancers, Dogo Asley, Shilole na bendi ya muziki wa dansi ya African Stars 'Twanga pepeta..
PICHA: ISSA MNALLY NA MUSSA MATEJA,/GPL
Habari hii ni kwa hisani ya Global Publishers

Wema

Monday, 13 February 2012

Wema anunuliwa gari baada ya kuachana na Diamond

Msanii wa filamu Bongo asiyeishiwa na matukio, Wema Sepetu amenunuliwa gari la kifahari na ndugu zake huku ikidaiwa kuwa ni pongezi kwa kuachana na mchumba wake, Naseeb Abdul ‘Diamond’.





Wema hivi karibuni aliliambia Risasi Jumamosi kuwa, gari hilo la shilingi milioni 35 aina ya Toyota Lexus lenye namba za usajili T 211 BXR, amenunuliwa na mama yake pamoja na ndugu wengine kufuatiakufurahishwa na uamuzi mgumu aliouchukua.






Awali kulikuwa na tetesi kuwa, gari hilo analotumia mrembo huyo kwa sasa amehongwa na mwanaume aliyechukua nafasi ya Diamond.




kazidi kudaiwa kuwa, lengo la mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina moja la Clemence kumnunulia Wema gari ni kumwepusha na vishawishi kutoka kwa wanaume mapedeshee.




“Lile gari analotembelea Wema kanunuliwa na yule jamaa yake wa sasa, si unajua tena mtoto mzuri kama yule hawezi kutumia daladala au teksi?” kilishadadia chanzo hicho ambacho ni rafiki wa Wema.








Wema afunguka
Akizungumzia madai hayo, Wema alisema wanaoamini amehongwa gari hilo wanakosea kwani ukweli ni kwamba amenunuliwa na ndugu zake kama zawadi.
“Najua kila mmoja atakuwa na lake la kusema juu ya hili gari ninalotumia kwa sasa, ukweli ni kwamba nimenunuliwa na mama na ndugu zangu wengine baada ya kutoka kwenye kashikashi zito na Diamond.
“Na mimi zaidi ya kuwashukuru pia naahidi kutowaangusha na nitajitahidi kutowakosea kwa namna yoyote ile,” alisema Wema.

Wema alikuwa mpenzi baadaye mchumba wa Diamond lakini hivi karibuni wawili hao walitibuana huku pia kukiwa na madai kuwa baadhi ya ndugu wa Wema

Habari kwa hisani ya: http://www.frednjeje.blogspot.com na