
NYOTA wa sinema za Kibongo, Rose Donatus Ndauka ameruka kimanga madai kwamba, amebadili dini kwa sababu ya kufuata ndoa, Risasi Jumamosi lina sauti yake mkononi.
Akizungumza juzikati jijini Dar es Salaam, Rose ambaye sasa anaamini katika Uislam alisema amefuata dini ya mama yake mzazi na si vinginevyo.

“Nilitaka kufanya hivyo siku nyingi lakini sasa naona ni muda muafaka ili niwe sambamba na mzazi wangu,” alisema staa huyo wa filamu ya Mahabuba.
Kauli za wadau wa filamu za Bongo kudai msanii huyo alibadili dini na sasa anaitwa Aisha lengo awe sare kwenye ndoa, zilitolewa mara baada ya Rose kuposwa na Marik Bandawe ‘Chiwa’ ambaye ni Muislam.
Rose anatarajia kufunga ndoa mapema mwezi Mei, 2012 baada ya kufanyiwa Kitchen Party na Send Off ya nguvu mwezi Aprili, jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment