YANGA YALAZIMISHWA KUONGEA KIARABU NA ZAMALEK UWANJA WA TAIFA

Wachezaji wa timu ya Yanga wakishangilia mbele ya mashabiki wao mara baada ya mchezaji wa timu hiyo Khamis Kiiza, kuifungia timu hiyo goli la kuongoza katika kipindi cha kwanza,Tayari mpira umekwisha na timu ya Zamalek imefanikiwa kusawazisha goli na kufanya matokeo kuwa 1-1 mpaka mwisho wa mchezo.Huu ni mchezo wa mashindano ya Klabu bingwa barani Africa yanayoandaliwa na shirikisho la vyama vya mpira wa miguu (CAF), timu hizo zitarudiana tena nchini Misri baada ya wiki mbili zijazo.
Mmoja wa wachezaji wa Yanga akipiga mpira kuelekea lango la Zamalek huku mlinda mlango wa timu hiyo akijaribu kuzuia ili mpira huo usilete madhara katika lango lake.
Mashabiki wa timu ya Yanga wakiwa wamevamia kweny jukwaa la Simba ambalo mashabiki wa Simba wanakaa.Chanzo: Kapingaz blog


No comments:
Post a Comment