BURIANI WHITNEY HOUSTON
Utakumbukwa daima
Katika maisha yangu kumuenzi na kumkumbuka Whitney houston, sitaweza kuisahau hoteli ya "Bevelley Hills Hotel" mahali ambapo uhai wa Whitney ndipo uliishia.
Kwanza kabisa nilipigwa na butwaa na kushindwa kuyaamini masikio yangu nilipozipata habari za kusikitisha za kifo cha mwanamuziki nguli duniani katika miondoko ya Soul na Rn'B Whitney Houston.
Kamwe dunia nzima haitaweza kumsahau Whitney kutokana na mchango wake mkubwa katika kuukuza na kuuendeleza muziki wa Soul na Rn'B duniani.
Alikuwa amepangwa kutumbuiza katika tuzo maarufu za muziki za Marekani ziitwazo "Grammy"
Ilikuwa ni wakati mgumu kwa Bobby Brown mara habari za kifo cha Whitney zilipomfikia. Wakati huo Bobby alikuwa Mississippi akifanya tamasha.
Sina imani kwamba pengo lake litaweza kuzibwa kwa urahisi kutokana na kipaji kikubwa alichojaliwa mwanadada huyu.
Ukiachilia mbali kashfa mbali mbali za matumizi ya madawa ya kulevya, kuna mambo mazuri aliyoyafanya Whitney ambayo tunaweza tukajifunza na kumuenzi kwayo.
Whitiney Houston alizaliwa mwaka 1963. Amekufa akiwa na umri wa miaka 49.Whitney houston ameacha mtoto mmoja ambaye amezaa na Bobby Brown.
Nikiwa kama mdau wa tasnia hii ya muziki napenda kuchukua nafasi hii kumuombea Hayati Whitney Houston alazwe mahali pema peponi .... Amen!
Sema chochote juu ya kifo cha Whitney Houston
ReplyDelete