ZAMBIA WATIMIZA AHADI
Ni mabingwa AFCON 2012
Libreville
TIMU ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Zambia maarufu
kama ‘Chipolopolo’ imetimiza ahadi iliyoitoa juzi wakati wakiwakumbuka
wachezaji wenzao waliokufa kwa ajali ya ndege mwaka 2003, kwa kutwaa
ubingwa wa Mashindano ya Fainali ya Kombe la Afrika (AFCON) leo.
Chipolopolo imefanikiwa kutwaa kombe hilo baada ya kuwafunga timu ya
Taifa ya Ivory Coast kwa mabao nane kwa saba (8-7) katika mikwaju ya
penati. Juzi kabla ya fainali hiyo mjini Libreville timu ya Zambia
ilitembelea eneo ambalo wenzao walipata ajali kwa kuwakumbuka na hivyo
kuwaahidi mashabiki wake kuwa itatwaa ubingwa ili kuwaenzi wachezaji
wenzao ambao walipata ajali ya ndege 1993 na kufariki wote.
Mpambano huo wa fainali ulikuwa mkati na mgumu kwa pande zote tofauti
na ilivyotarajiwa labda Ivory Coast ingepata unafuu kutokana na kuwa na
mastaa wengi wanaochezea ligi kubwa ulimwenguni.

Stophira Sunzu wa Zambia ndiye muuaji wa Timu ya Taifa ya Ivory Coast katika Mashindano ya Fainali za Afrika mchezo wa fainali.
Zambia walionesha upinzani mkubwa katika dakika zote, ambapo timu zote zilishambuliana kwa zamu kila wanapopata nafasi. Mchezaji Didie Drogba huenda atakuwa wakwanza kulaumiwa baada ya kukosa penati iliyokwenda nje ndani ya dakika 90 za mchezo.
Hadi dakika 90 zinamalizika timu zote zilikuwa sare 0-0 na kuongezewa
dakika 30 ambazo pia hakuna aliweza kukwamisha mpira katika nyavu za
goli la mpinzani wake. Baada ya muda huo zilipigwa penati ambapo ndipo
Zambia walifanikiwa kuwa mabingwa wa AFCON.
Muuaji wa Ivory Coast ni beki wa Zambia, Stophira Sunzu aliyefunga
penati ya mwisho baada ya wapinzani wao kukosa, hivyo kuifanya timu yake
kuibuka na magoli 8-7 dhidi ya Ivory Coast. Hadi mwisho wa pambano
Chipolopolo 8 na Ivory Coast 7. Kwa ushindi huo Chipolopolo ya Zambia
imetawazwa mabigwa huku Ivory Coast ikishika nafasi ya pili na Timu ya
Taifa ya Mali ikishika nafasi ya Tatu baada ya kuitoa Ghana Jumamosi.
No comments:
Post a Comment