For home theatre system solution

Thursday, February 16, 2012

MBEYA

BASI LA HAPPY NATIONAL LAPATA AJALI MKOANI MBEYA




Basi la Happy Nation limeanguka baada ya kushindwa kuumudu mteremko wa TAZAMA, maarufu kama Pipeline. 
 
Habari toka kwa abiria waliopanda basi la Nganga, wanasema watu wamejeruhiwa vibaya ila hakuna vifo. 
 
Basi hilo likiwa kwenye mwendo kasi lilitaka kulipita basi la Nganga, lakini kukawa na gari jingine linapandisha mlima huo, ndipo dereva akalazimika kulirudisha nyuma ya basi la Nganga na kuligonga kwa nyuma na kupinduka.
 
Abiria wa basi la Nganga wamesalimika wote.
 
Picha na Felix Mwakyembe
Habari hii ni kwa hisani ya http://www.latestnews.blogspo.com

No comments:

Post a Comment