Kesi ya ulanguzi yamuandama Rais Zuma
Chama cha Democratic alliance kinasema kuwa uamuzi wa mwendesha mashataka wakati huo wa kuondoa mashataka dhidi ya Rais Jacob Zuma ulichukuliwa kwa misingi ya kisiasa na sio kisheria.

Anakabiliwa na tuhuma za kuhusika na ulanguzi
Katika kipindi hicho mkuu wa kitengo maalum cha upelelezi cha polisi maarufu kama scorpions na mwendesha mashtaka walidaiwa kufanya njama ya kummaliza kisiasa Rais Zuma.
Kanda za mazunguzmo hayo kati yao zilitumika mahakamani kama ushahidi wa njama hiyo.
Mwaka wa 2007, Jacob Zuma alifunguliwa mashataka ya kuhusika na rushwa, udanganyifu na ulanguzi.
Kesi hiyo dhidi yake iliwasilishwa siku nane baada ya kumshinda aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki kwenye mvutano wa kukiongoza chama cha ANC.
Mashtaka hayo yaliibuka baada ya aliyekuwa mshauri wa masuala ya kiuchumi wa Zuma, Shabir Shaik alipopatikana na hatia ya ulanguzi.
Mshataka dhidi ya Zuma yaliondolewa, wiki mbili kabla uchaguzi wa April mwaka 2009. Hatua hiyo iliwaudhi viongozi wa upinzani na baadhi ya mashirika ya kijamii huko Afrika kusini.
Wakosoaji wanasema lazima mahakama iamue ikiwa kweli kiongozi huyo alikuwa na hatia. Kwa hivyo uamuzi wa mahakama kuu kuhusu kesi hii unasubiriwa kwa hamu.
No comments:
Post a Comment