Moto wateketeza gereza na kuua watu 272 Honduras
Moto mkubwa umetokea katika gereza moja nchini Honduras na kuua takriban wafungwa 272,wengi wao wameteketea wakiwa kwenye seli zao.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya Lucy Marder, mkuu wa idara ya uchunguzi wa sababu za kifo katika ofisi ya waendesha mashtaka. Mkuu wa magereza Danilo Orellana amesema moto huo, ambao chanzo chake bado hakijajulikana, ulitokea jana usiku katika mji wa Comayagua, kilomita 140 Kaskazini mwa mji mkuu wa Honduras.
Akielezea janga hilo mara tu baada ya kufika gerezani hapo, msemaji wa kikosi cha zima moto, Josue Garcia amesema aliona picha za ajabu zinazotisha kama za kishetani wakati akijaribu kuzima moto huo.
Gereza hilo lina kiasi ya wafungwa , 800 na wakati baadhi wakifanikiwa kutoroka zaidi ya wafungwa 100 walikufa papo hapo baada ya kushindwa kujiokoa kwani mlinzi aliyekuwa na ufunguo haikujulikana aliko.

No comments:
Post a Comment